TAMBUA SABABU
ZINAZOWEZA KUPELEKEA KUTOKUFANIKIWA
KWA MALENGO YAKO ULIYOJIWEKEA
KWA MWAKA 2018
Nipende kumshukuru mwenyezi
Mungu kwa kutowezesha kuingia katika mwaka
mpya wa
2018.Pia nikupongeze wewe kwa
kuweza kuwa miongoni mwa waliopewa
nafasi nyingine na Mungu kuingia mwaka 2018.
Imekuwa kawaida na mazoea
kila mtu kuweka malengo yake mwishoni au mwanzoni mwa
mwaka kwaajili ya maisha yake na vizazi yake vya baadaye.Hata hivyo watu wengi hushindwa kutimiza malengo yao kwa sababu
mbalimbali.
Zifuatazo ni sababu
zinazopelekea malengo waliojiwekea watu
walio wengi kutotimia;
1. KUTOKUANDIKA MALENGO
(UNWRITTEN GOALS);
Watu wengi wamekuwa na malengo yaliyowekwa kichwani badala
ya kuyaandika sehemu maalum ili iwe rahisi kupitia kila siku na kujua nini
wanapaswa kufanya .Kuweka malengo
kichwani ni rahisi kupotea na hutoweza kukumbuka kila kitu ulichokuwa umekipanga.
Leo amua kubadilika
na kuanza kuandika malengo kwenye notebook yako,kwenye kompyuta yako,kwenye
simu yako na unaweza kwenda mbali zaidi
ukayahifadhi mtandaoni hasa kwa njia ya email au vihifadhi vingine kama vile
Googledrive ,Dropbox nakadhalika.
2. KUTOWEKA
VIPAUMBILE (LACK OF PRIORITIZATION);
Ukiweka malengo ,ukayaandika
lakini ukashindwa kuweka vipaumbele ni wazi kuwa hutoweza kufikia
malengo yako.Vipaumbele hutoa mwelekeo wa nini unapaswa kuanza nacho na kwa
nini ,Wakati unapokuwa na lengo zaidi ya moja ni muhimu kukaa chini na
kuangalia nini kianze kwa kuangalia umuhimu wake na rasilimali ulizonazo kwa wakati
huo.Usipokuwa na vipaumbele utafanya chochote na muda mwingine hata yale ambayo
hayako kwenye malengo yako uliyojiwekea.
3.KUTOWEKA UKOMO WA
MUDA(NO TIME FRAME/UNBOUNDED GOALS);
Kama umeweka malengo
na malengo hayo yasiwe na ukomo
wa muda ni wazi kwamba huwezi kufikia malengo yako.Utakuwa ni mtu wa kusema
nitafanya kesho,Kesho kutwa au hata mwakani kwa sababu hukuweka ukomo wa
malengo yako.Ni vema sana ukaanza sasa kuweka muda wa kukamilisha kila lengo
nah ii itakusaidia katika kukamilisha malengo yako.
4.KUTOKUWA NA MALENGO
HALISIA (UNREALISTIC GOALS);
Kuna watu wanaweka malengo kwa kujifurahisha tu bila
kuangalia uhalisia wa malengo hayo kama kweli ni malengo yanayoweza kufikika.Ni
muhimu wakati wa kuweka malengo yako
hisia zako ziwe mbali sana.Weka malengo halisi ambayo unaamini yanawezekana
baada ya kupima uwezo ulionao.Acha kuweka malengo kwa kunakili au kuiga kwa
watu wengine bali weka malengo yako halisia.
5.KUTOKUWA NA MPANGO
KAZI KWA KILA LENGO (LACK OF ACTION
PLAN);
Kuweka lengo tu haitoshi,ni muhimu ukaandaa mpango kazi kwa
lengo.Kwa mfano umepanga kuanzisha kampuni mwaka huu ni lazima katika lengo
hilo utengeneze mpango kazi utakaoeleza
vyanzo vya pesa vya kuanzisha kampuni
hiyo,Watu wanaohitajika katika mchakato ,wahusika wa usajili kama vile
wanasheria nakadhalika.Kama hutafanya mambo hayo kwa ufasaha na weledi wa hali
ya juu ni vigumu sana kufikia malengo yako ya kuanzisha kampuni.
6.KUTOKUTILIA
MANANI(LACK OF COMMITMENT/SERIOUSNESS);
Kama umeweka malengo na hautilii manani hakuna
kitakachotokea na mwisho wa siku utakuja na sababu nyingi pamoja na
visingizio vingi vilivyosababisha
kutokufikia malengo yako,kumbe wewe ndiwe uliyesababisha malengo yako
kutotimia.Ni muhimu sana kama unataka kufika mahali unapotaka kufika ukajenga
utamaduni wa kutilia maanani kila ulifanyalo.Hayo ni maisha yako na wewe ndiye
nahodha wa maisha yako mwenyewe na si
mwingine kumbuka maisha yako yapo
mikononi mwako mwenyewe.Kama utafanya uvivu ama ulegevu,nakuhakikishia kuwa
hautatoka kwenye maisha hayo mpaka pale utakapobadilika.
7. KUTOSHIRIKISHA
MALENGO(SELFISHNESS/EGOISM);
Watu wengi wanaweka malengo na hawaweki wazi kwa watu
wengine huku wakisema malengo ni siri.Iko hivi kama utajiwekea malengo na
ushimshirikishe mtu yeyote ni ngumu sana kufikia malengo yako.Unapomshirikisha
mtu sahihi malengo yako yeye anaweza kukushauri nini unaweza kufanya na kwa
namna ipi ili uweze kufikia malengo yako.Acha kukaa na malengo yako bila
kumwambia mtu yeyote ni hatari sana na hutakuwa na msukumo wa
kuyafikia maana hakuna anayejua.
8.KUTOFANYA
TATHMINI(LACK OF EVALUATION);
Kama huna utaratibu wa kukaa chini na kujua nini
kimefanyika mpaka sasa ni ngumu sana
kuja kufikia malengo yako maana hutajua
nini kimefanyika na kipi bado hakijafanyika na kifanywe kwa namna ipi.Ni muhimu
sasa kama unataka kufika mbali ukaanza kufanya tathmini ya nini umefanya na
wapi umeshindwa na kujua na suluhisho
kama kuna changamoto yoyote imejitokeza.
Nakutakia kila la heri katika kukamilisha malengo yako
uliyojiwekea katika mwaka huu wa 2018.Usikate tamaa,Usiogope wala usirudi nyuma
katika mapambano ya kufikia malengo yako uliyojiwekea(ALUTA CONTINUA)
Makala hii
imeandaliwa na kuandikwa na ;
Samwel Mohabe Marwa
Mbusiro(Mwalimu,Mwinjilisti,Mhubiri ,Mwandishi,Mwanaharakati,Kiongozi ,Mhamasishaji,
pamoja na Mzungumzaji mbele ya halaiki au mhadhara)-Mwanafunzi
chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili(MUHAS)
Simu: 0745325I74/0719200317
Barua pepe : samwelmarwa88@gmail.com
Blog:samwelmohabe.blogspot.com
Sanduku la posta: S.L.P 65001 Dar es salaam,Tanzania
23/02/2018.