Thursday, February 22, 2018

TAMBUA SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA KUTOKUFANIKIWA KWA MALENGO YAKO ULIYOJIWEKEA KWA MWAKA 2018TAMBUA SABABU ZINAZOWEZA   KUPELEKEA  KUTOKUFANIKIWA  KWA  MALENGO YAKO   ULIYOJIWEKEA  KWA  MWAKA  2018

Nipende kumshukuru mwenyezi  Mungu kwa  kutowezesha  kuingia  katika  mwaka  mpya  wa  2018.Pia nikupongeze  wewe  kwa  kuweza  kuwa  miongoni  mwa  waliopewa nafasi  nyingine na Mungu  kuingia mwaka 2018.
Imekuwa kawaida na mazoea  kila mtu kuweka malengo yake mwishoni au mwanzoni  mwa  mwaka kwaajili ya maisha yake na vizazi yake vya baadaye.Hata  hivyo watu wengi  hushindwa kutimiza malengo yao kwa sababu mbalimbali.
Zifuatazo ni sababu  zinazopelekea malengo waliojiwekea watu  walio wengi  kutotimia;

1. KUTOKUANDIKA MALENGO (UNWRITTEN GOALS);
Watu wengi wamekuwa na malengo yaliyowekwa kichwani badala ya kuyaandika sehemu maalum ili iwe rahisi kupitia kila siku na kujua nini wanapaswa kufanya .Kuweka malengo  kichwani ni rahisi kupotea na hutoweza kukumbuka kila  kitu ulichokuwa umekipanga.
Leo  amua kubadilika na kuanza kuandika malengo kwenye notebook yako,kwenye kompyuta yako,kwenye simu yako  na unaweza kwenda mbali zaidi ukayahifadhi mtandaoni hasa kwa njia ya email au vihifadhi vingine kama vile Googledrive ,Dropbox  nakadhalika.

2. KUTOWEKA VIPAUMBILE (LACK OF PRIORITIZATION);
Ukiweka malengo ,ukayaandika  lakini ukashindwa kuweka vipaumbele ni wazi kuwa hutoweza kufikia malengo yako.Vipaumbele hutoa mwelekeo wa nini unapaswa kuanza nacho na kwa nini ,Wakati unapokuwa na lengo zaidi ya moja ni muhimu kukaa chini na kuangalia nini kianze kwa kuangalia umuhimu wake na rasilimali ulizonazo kwa wakati huo.Usipokuwa na vipaumbele utafanya chochote na muda mwingine hata yale ambayo hayako kwenye malengo yako uliyojiwekea.

3.KUTOWEKA UKOMO WA MUDA(NO TIME FRAME/UNBOUNDED GOALS);
Kama umeweka malengo  na malengo  hayo yasiwe na ukomo wa muda ni wazi kwamba huwezi kufikia malengo yako.Utakuwa ni mtu wa kusema nitafanya kesho,Kesho kutwa au hata mwakani kwa sababu hukuweka ukomo wa malengo yako.Ni vema sana ukaanza sasa kuweka muda wa kukamilisha kila lengo nah ii itakusaidia katika kukamilisha malengo yako.

4.KUTOKUWA NA MALENGO HALISIA (UNREALISTIC GOALS);
Kuna watu wanaweka malengo kwa kujifurahisha tu bila kuangalia uhalisia wa malengo hayo kama kweli ni malengo yanayoweza kufikika.Ni muhimu wakati wa kuweka malengo  yako hisia zako ziwe mbali sana.Weka malengo halisi ambayo unaamini yanawezekana baada ya kupima uwezo ulionao.Acha kuweka malengo kwa kunakili au kuiga kwa watu wengine bali weka malengo yako halisia.

5.KUTOKUWA NA MPANGO KAZI KWA  KILA LENGO (LACK OF ACTION PLAN);
Kuweka lengo tu haitoshi,ni muhimu ukaandaa mpango kazi kwa lengo.Kwa mfano umepanga kuanzisha kampuni mwaka huu ni lazima katika lengo hilo utengeneze mpango kazi  utakaoeleza vyanzo  vya pesa vya kuanzisha kampuni hiyo,Watu wanaohitajika katika mchakato ,wahusika wa usajili kama vile wanasheria nakadhalika.Kama hutafanya mambo hayo kwa ufasaha na weledi wa hali ya juu ni vigumu sana kufikia malengo yako ya kuanzisha kampuni.

6.KUTOKUTILIA MANANI(LACK OF COMMITMENT/SERIOUSNESS);
Kama umeweka malengo na hautilii manani hakuna kitakachotokea na mwisho wa siku utakuja na sababu nyingi pamoja na visingizio  vingi vilivyosababisha kutokufikia malengo yako,kumbe wewe ndiwe uliyesababisha malengo yako kutotimia.Ni muhimu sana kama unataka kufika mahali unapotaka kufika ukajenga utamaduni wa kutilia maanani kila ulifanyalo.Hayo ni maisha yako na wewe ndiye nahodha wa maisha yako  mwenyewe na si mwingine kumbuka maisha yako  yapo mikononi mwako mwenyewe.Kama utafanya uvivu ama ulegevu,nakuhakikishia  kuwa  hautatoka kwenye maisha hayo mpaka pale utakapobadilika.

7. KUTOSHIRIKISHA MALENGO(SELFISHNESS/EGOISM);
Watu wengi wanaweka malengo na hawaweki wazi kwa watu wengine huku wakisema malengo ni siri.Iko hivi kama utajiwekea malengo na ushimshirikishe mtu yeyote ni ngumu sana kufikia malengo yako.Unapomshirikisha mtu sahihi malengo yako yeye anaweza kukushauri nini unaweza kufanya na kwa namna ipi ili uweze kufikia malengo yako.Acha kukaa na malengo yako bila kumwambia  mtu yeyote ni  hatari sana na hutakuwa na msukumo wa kuyafikia maana hakuna anayejua.

8.KUTOFANYA TATHMINI(LACK OF EVALUATION);
Kama huna utaratibu wa kukaa chini na kujua nini kimefanyika  mpaka sasa ni ngumu sana kuja kufikia malengo  yako maana hutajua nini kimefanyika na kipi bado hakijafanyika na kifanywe kwa namna ipi.Ni muhimu sasa kama unataka kufika mbali ukaanza kufanya tathmini ya nini umefanya na wapi umeshindwa  na kujua na suluhisho kama kuna changamoto yoyote imejitokeza.

Nakutakia kila la heri katika kukamilisha malengo yako uliyojiwekea katika mwaka huu wa 2018.Usikate tamaa,Usiogope wala usirudi nyuma katika mapambano ya kufikia malengo yako uliyojiwekea(ALUTA CONTINUA)


Makala hii imeandaliwa na kuandikwa  na ;
Samwel  Mohabe Marwa Mbusiro(Mwalimu,Mwinjilisti,Mhubiri ,Mwandishi,Mwanaharakati,Kiongozi ,Mhamasishaji, pamoja  na  Mzungumzaji mbele ya halaiki au mhadhara)-Mwanafunzi chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili(MUHAS)
Simu: 0745325I74/0719200317
Blog:samwelmohabe.blogspot.com
Sanduku la  posta: S.L.P  65001 Dar es salaam,Tanzania
                    23/02/2018.

Saturday, April 29, 2017

MAJERAHA YA NAFSI PART TWO


KARIBUNI KATIKA SEHEMU YA PILI YA SOMO HILI

ZITAMBUE SIFA/TABIA  ZA NAFSI

Nafsi ni sehemu ya mwanadamu inayosababisha  mwanadamu kuwa hai,yaani kinachokufanya wewe ulivyo leo ni nafsi yako.
Mwanzo 2:7 Biblia inasema''Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu  akawa NAFSI HAI''

Zifuatazo ni sifa au tabia za   NAFSI

1.KWENYE NAFSI NDIPO KUNATOKA MAAMUZI YAKO WEWE(DECISION MAKING)

Zaburi 11:5 ''Bwana humjaribu mwenye haki bali nafsi yake humchukia asiye haki,na mwenye kupenda udhalimu''

kwenye nafsi ya mtu ndipo maamuzi hutokea,ndugu msomaji hakuna maamuzi yoyote uliwahi kuyafanya pasipo msukumo kutoka NAFSINI mwako,kama ulikuwa hujui tambua hilo leo.

Mwanadamu ameundwa na vitu vitatu ambavyo ni
A)MWILI
B)NAFSI
C)ROHO

Ndugu kuna muda unaweza kutamani jambo fulani baya katika maisha yako lakini nafsi yako ikakusuta na ukaacha kufanya hilo jambo,Wakati mwingine mwili ulikudanganya kuiba pesa kwa mtu fulani ,lakini nafsi yako ilisema hapana.Ukiona umemtamani mwanamke au mwanaume wa mtu ili uzini naye/ulale naye/ufanye naye mapenzi na ukafanikiwa kuzini naye jua kuwa hapo nafsi yako ilikuwa dhaifu kwenye maamuzi ,iko hivi mwili siku zote hutamani ukishindana na roho,hivyo kama MWILI ukiwa na nguvu kuliko ROHO hivyo nafsi hutekeleza matakwa ya mwili na kama  Roho itakuwa na nguvu kuliko vilevile nafsi itaamua matakwa ya Roho,NAFSI KAZI YAKE KUBWA NI KUFANYA MAAMUZI KATIKA YA ROHO NA MWILI NA KILE AMBACHO NAFSI HUTEKELEZA ADHIMA YAKE KAT YA ROHO NA MWILI JUA HICHO KINANGUVU KULIKO MWENZAKE.


2.KWENYE NAFSI NDIPO KUNATOKA FIKRA(MIND/UNDERSTANDING)

Mithali 23:7a ''Maana aonavyo NAFSINI mwake ndivyo alivyo''

Ukiona katika maisha yako unafikra mbaya juu yako mwenyewe au juu ya mwingine tambua kuwa nafsi yako haijakombolewa bado inahitaji kukombolewa.Yawezekana umewahi kuona kwa kuambiwa na nafsi yako kuwa huwezi kufanikisha jambo fulani hivyohivyo na wewe ukakata tamaa juu ya jambo hilo moja kwa moja.KINACHOTAKIWA KWENYE MAISHA YAKO NI KUIAMBIA NAFSI YAKO KUWA KILA KITU UNAWEZA HATA KAMA HUJUI JINSI YA KUKIWEZA.

Yoeli 10b 'ALIYEDHAIFU NA ASEME ,MIMI NI HODARI''.Hata kama ukiwa mnyonge na dhaifu iambie nafsi yako kuwa unaweza,nafsi huwa ya aina fulani kutokana na vyakula inavyolishwa mfano wewe kila siku ukilisha nafsi yako kuwa huwezi ndugu niamini HAUTAWEZA KWELI.Penda kulisha nafsi yako mawazo mema,mawazo ya ushindi na ya mafanikio,kuwa na tambia ya kuiambia nafsi yako kuwa kila jambo linawezekana na unaweza ukalifanya hata kama wengine hawakulifanikisha ,NAFSI MARA NYINGI HUDANGANYIKA BAADA YA KUONA MTU FULANI AMBAYE AMEFANYA JAMBO FULANI HALIJAFANIKIWA HUKULETEA PICHA KUWA WEWE HUWEZI HILI JAMBO MAANA FULANI LIMEMSHINDA WEWE UTAWEZAJE HIVYO HUKULETEA HOFU NZITO NA USIPOKUWA MAKINI NAFSI HUKUSHINDA

3.KWENYE NAFSI NDIPO  KUNATOKA HISIA (EMOTIONS/FEELINGS)

siku zote nafsi yako inapenda ipendwe,isifiwe,ipongezewe,ikubalike,ipewe fursa

Fuatilia mfano huu utaelewa kitu nasema ,UKIWA UNATEMBEA UKAPITA KATIKATI YA KUNDI LA WATU WAMEKAA WANAZUNGUMZA  KUKAWA KUNA MTU UNAMFAHAMU HALAFU UKAMSALIMIA KWA MARA YA KWANZA LAKINI YEYE AKAKAA KIMYA AIDHA KWA KUSIKIA AU KUTOKUSIKIA,UTAJARIBU KUPAZA SAUTI ILI AKUSIKIE,PALE AMBAPO HAKUKUJIBU NINI KILITOKEA NI JERAHA KATIKA NAFSI YAKO MAANA NAFSI YAKO HUJIONA KAMA UMEDHAURIKA,HAKUKUJALI,HAKUPENDI HAYO YOTE YANATOKEA MAANA NAFSI HUTAMANI KUFANYIWA MEMA ,KUJALIWA NA KUPENDWA.NDIO MAANA KATIKA KUNDI ULILOPITA KAMA KUNA WATU WANAFIKRA NZURI UTASIKIA WANAKUAMBIA USIJALI BWANA HAJASIKIA AU POLE HAJASIKIA.kwa nini watakwambia kwa sababu wanajua nafsi imetendewa vitu ambayo haipendi. VITU VINAVYOJERUHI NAFSI ZA WATU WALIOWENGI NA KUWAACHIA MAJERAHA


1.MAHUSIANO

Siku moja Dada mmoja aliniambia kuwa wanaume wote anawachukia na hataki hata kuwaona,Roho mtakatifu akaniambia kuwa amejeruhiwa nafsi yake na wanaume hao ndio maana hataki kuwaona.Ndipo nikapata ujasiri wa kumuuliza kwanini akaanza kunielezea namna ambayo kaka mmoja waliyekuwa wameahidfiana kuwa wachumba na wakawa wachumba kweli ila yule mkaka mwisho wa siku akamuacha yule mdada na akampata mdada mwingine hivyo nafsi ya dada yule ikajeruhiwa na ikamwambia fanya maamuzi ya kuchukia wanaume wote,kila mwanaume unayemuona dunia Muone kama kiumbe hatari kwako.


2.MARAFIKI
kuna watu wameumizwa nafsi zao kutokana na aina ya marafiki waliochagua kuwa nao katika maisha yao,kuna wengine marafiki zao walitembea na mume wake au mke wake,kuna wengine marafiki zao waliwashawishi kuwa na tabia za wizi,kuna wengine marafiki zao waliwasababisha wakafeli masomo yao,kuna wengine marafiki zao waliua ndoto zao walizokuwa nazo.Rafiki yako anaweza akawa Adui yako mkubwa au rafiki yako mkubwa maana huwa anajua siri zako kuliko mtu yeyote,huwa anajua maono na ndoto zako kuliko mtu yeyote hivyo kuwa makini katika uchaguzi wa marafiki la sivyo utapelekea nafsi yako kupata majeraha makubwa sana ambayo kuyaziba itahitaji muda mwingi na gharama nyingi sana

Zekaria 13:6''NA MTU ATAMWAMBIA ,JE JERAHA HIZI ULIZONAZO KAIKA YA MIKONO YAKO NININI,NAYE ATAJIBU,NI JERAHA NILIZOTIWA KATIKA NYUMBA YA RAFIKI ZANGU''3.WAZAZI/WALEZI WAKO
kuna wengine nafsi zao zimejeruhiwa kutokana na malezi waliyoyapata kutoka kwa wazazi au walezi wao.Yawezekana ulikua katika mazingira ambayo wazazi wako wote walikuwa wamefariki,hivyo nafsi yako ikawa yamasononeko ,majonzi na huzuni muda wote  au kuna wengine ambayo wamelelewa na wazazi katika mazingira ya kuwabana sana(WATOTO WA GETI KALI)yaani haupati hata muda wakutoka ufurahi na wenzako,ucheke na wenzako ,uimbe na wenzako ,hivyo nafsi yako huwa ya kubanwa na uoga siku zote,Kumbuka nimekuambia nafsi hupenda kufurahi,kuchangamka na kuwa huru hivyo basi nafsi hujeruhiwa na wazazi.WEWE MZAZI UNAYESOMA UJUMBE HUU KUMBANA MTOTO WAKO NDANI YA GETI SIKU ZOTE SIO NJIA YA KUMFANYA MTAKATIFU AU YA KUMZUIA KUFANYA MAOVU BALI NI NJIA YA KUIANGAMIZA NAFSI YAKE NA KUATHIRI MFUMO WAKE WA FIKRA,NJIA RAHISI YA KUMFUNDISHA MWANAO KUACHA MAOVU NI KUMFUNDISHA NENO LA MUNGU KWA WINGI NA KUMUACHA KUWA HURU.
4.NDUGU ZAKO
Kuna watu wameumizwa na ndugu zao nafsi zao,na kupelekea muda mwingine kutokusalimiana,kuongea,kushiriki meza moja,kushiriki ibada moja,kushiriki chakula pamoja,kushikana mikono na kadhalika.ukiona watu kama hawa ikiwa ni wewe mwenyewe au katika jamii yako jua kuwa kuna watu nafsi zao zimejeruhiwa tayari5.MUAJIRI WAKO
kuna watu ambao katika kazi zao kila siku wanamgogoro na muajiri wake,inaweza kuwa ni kwa sababu ya maslahi,wivu ,madaraka,mshahara au cheo.utakuta Bosi hawasalimiani na muajiriwa wake.ukiona watu kama hao kazi jua kuwa kuna mmoja wapo aidha BOSI AMA MUAJIRIWA AMEJERUHIWA NAFSI YAKE.Vitu vinavyosababisha nafsi za waliowengi wengi kujeruhiwa ni vingi sana ila kwa leo naomba kuisha hapo.ILI KUPONYA NAFSI INAHITAJI TUMUAMINI MUNGU KUPITIA MWANAYE YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU KWA SABABU NAFSI NI SEHEMU YA MWANADAMU AMBAYO MUNGU ALIIUMBA KWETU,HIVYO ILI IPONYE INAHITAJI MUUMBA WAKE AIPONYE.

Hosea 6:1 ''Njoni ,tumrudie BWANA;maana yeye amerarua,na yeye atatuponya ;yeye amepiga,na yeye atatufunga JERAHA ZETU''.


NINAWATAKIA USOMAJI MWEMA NA MUNGU WANGU AWABARIKI WOTE


MARWA SAMWEL M
0719200317/0745325174
samwelmarwa88@gmail.com
samwelmohabe.blogspot.com
P.O.BOX 65001
DAR ES SALAAM


GOD KINGDOM MINISTRY.

Friday, February 24, 2017

MAJERAHA YA NAFSI

KARIBU KWENYE SOMO HILI LA MAJERAHA YA NAFSI TUJIFUNZE WOTE.

NAFSI  ni ule uhai wa mtu (nafsi ndiyo wewe mwenyewe).Kinachokufanya kuishi wewe ni kwa sababu nafsi yako iko hai au ni kwa sababu nafsi yako inaishi.

Mwanzo 2:7 inasema Bwana akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai,mtu akawa nafsi hai

Yohana 10:11 inasema Mimi ndiye mchungaji  mwema.Mchungaji mwema huutoa UHAI wake kwaajili ya kondoo,YESU alisema kuwa yeye kwa sababu ni mchungaji mwema atatoa NAFSI yake au UHAI  wake afe kwaajili yetu wanadamu.

MAJERAHA ni ile hali mtu au kitu chochote kuumizwa na mtu mwingine au kitu kingine na kuachiwa maumivu makali sana ambayo ili kupona maumivu hayo mpaka yapewe tiba.

MAJERAHA YA NAFSI ni ile hali ya nafsi ya mwanadamu  au kitu chochote chenye nafsi  kuumizwa na mtu mwingine au kitu chochote ambapo ili majeraha haya yapone yanahitaji tiba.

KWANINI NIMEAMUA KUKULETEA SOMO HILI

Ndugu neno hili imekuwa msukumo mkubwa ambao MUNGU aliweka ndani yangu miaka 7  iliyopita tangu 2010 nikiwa   JIJINI MWANZA

ILIKUWA  mwaka 2010 mwezi wa 12 nikiwa MWANZA ambapo kuna dada mmoja aliyeitwa PILLY aliyekuwa ni mwanachuo wa chuo kikuu cha mtakatifu AUGUSTINO -MWANZA ,  Dada huyu alikuwa na kaka mmoja aliyeitwa kwa jina la JOSEPH watu hawa wawili waliahidiana kuoa yaani walikuwa wachumba wa Muda mrefu kama miaka 2 na alikuwa amebakiza mwaka wake wa mwisho wa kuhitimu elimu yake ya chuo kikuu.

SIKU moja huyo   mkaka alimwambia huyo mdada  kuwa yeye hayuko tayari kumuoa huyo binti .YULE BINTI baada ya kuambiwa hivyo alichukua uamzi wa kunywa sumu ili afe aondoke duniani maana aliona hana thamani tena hapa duniani akimkosa yule mkaka ,YULE MDADA ALIKUNYWA SUMU KWA SABABU NAFSI YAKE ILIKUWA IMEPATA MAJERAHA MAKUBWA( MAJERAHA YA NAFSI)
Ninamshukuru sana MUNGU kwa sababu  MUNGU alinitumia mimi kuokoa maisha ya yule dada,nilikuwa nipo nje ya Nyumba ambayo tulikuwa tunakaa ambapo mtoto mdogo wa miaka 9 alikimbia nje kwa haraka sana na kuniambia njoo uone dada ambavyo amekuwa.NDUGU nilivyoenda ndani yule mdada alikuwa akitoka MAPOVU  MDOMONI NA PUANI NA HUKU AKITAPIKA nikakimbia mpaka dukani kwa bwana mmoja aliyekuwa na duka jirani yetu kwa haraka sana pasipo hata hodi nikaingia ndani nikachukua MAZIWA pasipo hata kulipa pesa nikarudi kwa haraka sana huku ninakimbia ,Bwana aliyekuwa na duka alishangaa sana hali ile kwa siku ile na watu walinishangaa sana maana haikuwa kawaida yangu kufanya hivyo,Wengine walisema nimechanganyikiwa na kuwa kichaa KUMBE HAWAKUJUA NILIKUWA NAKIMBIA KUOKOA UHAI WA BINTI YULE.Nilipofika nilimnywesha MAZIWA yale kwa lazima ambapo alitapika ILE SUMU YOTE ALIYOKUWA AMEKUNYWA.Na baada ya tukio hilo nikampigia simu yule mkaka ALIYEMJERUHI i NAFSI YAKE NA KUMUELEZA YALIYOTOKEA AMBAPO ALIKUJA KWA HARAKA NA KUMPELEKA HOSPITALI.

MUNGU NI MWEMA yule dada alipona majeraha yake maana  yule mkaka aliyemjeruhi nafsi yake walisameheana  na kuoana  mwaka 28/4/2012 ambapo mpaka dakika hii ninayozungumza wana watoto wawili na wanaishi kwa furaha sana katika ndoa yao na wamekuwa mfano wa kuigwa katika jamii yao.
MTU MMOJA ASEME AMEN.


TABIA ZA MTU  ALIYEPATA MAJERAHA YA NAFSI

1.HUWA NA HASIRA AMBAZO HAZIISHI MUDA WOTE,mtu aliyejeruhusiwa nafsi yake huwa na hasira muda wote kwa watu wengine maana nafsi yake imeumizwa hata kumpelekea hasira
.
2. HUWA NA CHUKI.mtu aliyejeruhiwa nafsi huwa haishiwi na chuki muda wote huwa na chuki kwa  wenzake maana yawezekana wao ndio waliosababisha nafsi yake kuumizwa na hivyo huchukua uamzi wa kuwachukia ,muda mwingine hataki kuwaona.

3.HANA AMANI WAKATI WOWOTE,nafsi ya mtu iliyojeruhiwa na watu au kitu kingine tofauti na watu huwa haina AMANI hata kidogo.

4.HUWA NA UADUI,muda wote huwaona watu wengine maadui zake.

5.HASAMEHI WENGINE,Nafsi yenye majeraha huwa ni ngumu sana kutoa msamaha pale ambapo ukimkosea hata kidogo au hata kwa bahati mbaya.mfano unaweza ukamkanyaga mguu wake kwa bahati mbaya akakuchukia maisha yake yote.

6.HULIPIZA KISASI,mtu mwenye nafsi iliyojeruhiwa huwa ni mtu wa kulipiza visasi visasi siku zote.akikosewa kidogo hutafuta mbinu ya kulipiza kisasi.

7.HUWA NA WIVU USIOKUWA WA MAENDELEO.mtu aliyejeruhiwa nafsi yake huwa na wivu usiokoma nafsi mwake.ukitaka kufanikiwa kidogo hutafuta hata mbinu ya kuua mafanikio yako yako.

8.HANA FURAHA,nafsi iliyojeruhiwa siku zote huwa haina furaha maana huwa imejaa chuki,masimango,huzuni,hasira,masononeka,uadui na ugomvi muda wote.

9.HUWA HANA UVUMILIVU.mtu aliyejeruhiwa nafsi yake siku zote huwa si mtu wa kuvumilia mambo.

10.HANA HURUMA,nafsi yenye majeraha haiwi na huruma kwa wengine mfano kuna wengine waliopata ukimwi kwa bahati mbaya hivyo wanapogundua kuwa wanaishi na virusi vya ukimwi hufanya mbinu zozote hata kwa kubaka ili tu asife mwenyewe yaani aambukize na wengine.

11.HANA UPENDO.mtu ambaye amejeruhiwa nafsi yake tayari huwa si mtu wa upendo hata kidogo kwa wenzake maana huwaona wao kama visababishi vya majeraha yake hata kama si wao.

NDUGU UKIJIONA UNATABIA KAMA HIZO JUA NAFSI YAKO IMEJERUHIWA ,HIVYO ANZA KUPIGA HATUA YA KUIPONYA NAFSI YAKO ILI USIENDELEE KUISHI KWA MAJERAHA BALI UISHI KWA AMANI.
AYUBU 22:21 inasema kuwa mjue sana MUNGU ILI UWE NA AMANI NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUJIA

NDUGU UKIMUONA MWENZAKO ANATABIA KAMA HIZO JUA NAFSI YAKE IMEJERUHIWA HIVYO USIMCHEKE WA KUMUONGEA KWA WENZAKO BALI MSHAURI NA MUOMBEE MAANA WEWE NI SEHEMU KUBWA SANA KWAKE KATIKA KUPONYA NAFSI  YAKE ILIYOPATA MAJERAHA.

KUMBUKA UNAWEZA UKAJERUHIWA NAFSI YAKO NA BABA YAKO,MAMA YAKO,KAKA YAKO,DADA YAKO,MKE WAKO,RAFIKI YAKO,MPENZI WAKO,NDUGU YAKO WA KARIBU,JIRAHI YAKO ,MCHUNGAJI WAKO,WAFANYAKAZI WENZAKO NA HATA BOSI WAKO.

NJIA KUBWA YA KUSHINDA MAJERAHA YA NAFSI NI KUKUBALI KUSAMEHE WENGINE HATA KAMA WAMEKUKOSEA AU WAMEKUKWAZA,KUMBUKA USIPOKUWA MTU WA KUSAMEHE HUIBEBESHA NAFSI YAKO MZIGO MKUBWA WA CHUKI UNAOTEMBEA NAO HUKU UKIKUSUMBUA SIKU ZOTE.KUANZIA LEO ACHILIA WALE WOTE WALIOKUUDHI NAFSINI MWAKO ILI UISHI KWA FURAHA ,UPENDO NA AMANI.

TEMBELEA BLOG YANGU MARA KWA MARA ILI KUJIFUNZA MENGI .

EV.SAMWEL MOHABE MARWA
samwelmarwa88@gmail.com
samwelmohabe.blogspot.com
FB: SAMWEL MOHABE MARWA
0719200317
P.O.BOX 65001 DAR ES SALAAM,
TANZANIAThursday, February 16, 2017

SABABU ZA KUSUDI LA MUNGU KUTOKUFANIKIWA KWA WATU

SABABU ZA KUSUDI   LA  MUNGU KUTOKUFANIKIWA KWA WATU 

Ninakusalimia katika JINA LIPITALO MAJINA YOTE AMBALO NI JINA LA YESU KRISTO.

KARIBU TUJIFUNZE TENA KATKA SEHEMU YA PILI YA KUSUDI LA MUNGU KWETU SISI WANADAMU.

Leo tutaangalia kuhusu sababu zinazopelekea kusudi la MUNGU ndani ya maisha yetu sisi wanadamu lisifanikiwe.Zifuatazo ni mojawapo ya sababu zinazopelekea kusudi la MUNGU lisifanikiwe kwetu wanadamu.

1.KUSUDI LA MUNGU KUFANYIKA KABLA AU NJE YA MUDA.
kuna watu ambao MUNGU ameweka vitu vikubwa ndani yao,ila vitu vinashindwa kufanikiwa pale ambapo mubeba kusudi anapotaka kufanya jambo hilo kabla ya wakati wake au baada ya wakati ule kuisha na yeye anajaribu kulifanya,yawezekana kusudi la MUNGU ni  kuwa kiongozi ,lakini umeshindwa kutambua nyakati na majira ambayo MUNGU amekuweka kuwa kiongozi ,hivyo ukilazimisha uwe kiongozi kabla ya wakati wako wa kuwa kiongozi haujafika utaharibu kusudi la MUNGU la kukuweka wewe kuwa kiongozi na pia ukifanya nje ya muda ambao MUNGU alikuweka uwe kiongozi unaharibu pia kusudi la MUNGU kwako maana MUNGU amepanga muda fulani uwe kiongozi na muda fulani usiwe kiongozi.
MHUBIRI 3:1-8 ,Biblia inaniambia kuwa ''kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.HIVYO WEWE MSOMAJI NINAKUSHAURI KUTAMBUA WAKATI UPI NI SAHIHI KWAKO KATIKA KULITIMIZA NA KULIFANIKISHA KUSUDI LA MUNGU KWAKO.

2.VIPINDI MUHIMU VYA MAISHA kama vile wakati wa ujana, wakati wa kutafuta mchumba na   wakati wa Ndoa
Hivi ni vipindi vya kuwa navyo makini sana ndugu msomaji maana vinaweza kuua kusudi la MUNGU haraka sana kwako
A)WAKATI WA UJANA
Kipindi cha ujana ni kipindi ambacho watu waslio wengi huharibu maono ya MUNGU na  makusudi ya MUNGU katika maisha yao ,maana hiki ni kipindi ambacho vijana huwakwa na tamaa za miili yao.Vijana huwa na tamaa na mihemko ya miili yao sana na wengi hujikuta wameingiza katika mtego wa ibilisi na kufanya uzinifu,NISIKILIZE KWA UMAKINI SANA NDUGU MSOMAJI YUSUFU ANGELIFANYA UZINZI NA YULE MKE WA POTIFA ASINGELIWEZA KUWA WAZIRI MKUU KATIKA MISRI,KILICHOSABABISHA YUSUFU AKATIMIZA KUSUDI LAKE LA KUWA WAZIRI MKUU KATIKA MISRI NI KWA SABABU ALIIKIMBIA DHAMBI YA UZINZI.soma Mwanzo  39:7-15
ushauri wangu kwenu ni kuwa hauwezi ukawa mzinifu halafu MUNGU akakuandaa kubeba kusudi lake kubwa kwaajili yako na kwaajili ya watu wake wengine.

B)WAKATI WA KUTAFUTA MCHUMBA
Nisikilize kwa umakini sana ndugu yangu,watu wengi wameshindwa kufanikisha kusudi la MUNGU katika Maisha yao kwa kujichanganya sana katika kipindi cha kutafuta mtu sahihi wa kuishi  naye kwa maisha ya baadaye yaani mke au mme ,watu wengi wanatafuta wachumba kwa akili zao wenyewe pasipo kumshirikishi MUNGU kumbuka MUNGU alimpa ADAMU  mkewe HAWA kama msaidizi wake hivyo nasi wanaume tunapotafuta MKE yapaswa tumuulize sana MUNGU kuhusu mke sahihi.NI HERI KUACHA KUOA KULIKO KUKOSEA KUCHAGUA MTU SAHIHI KATIKA MAISHA YAKO maana utakuwa na majuto katika maisha yako yote.MKE KAMA MSAIDIZI KWA MWANAUME NI WA KUJA KUBEBA MAONO YAKO  WEWE MWANAUME.HIVYO UKIKOSEA MUBEBA MAONO YAKO KBALIANA NA MIMI TU KKUWA KUSUDI LA MUNGU KWAKO HAKIKA HALITAFANIKIWA MAANA ANAYEBEBA MAONO YAKO NAYE HAJAKAA SAWA MAANA UTAPANGA KUFANYA HIVI ATAKUAMBIA HIYO HAIFAI NA UTAMSIKILIZA NA KUFANYA KINYUME NA KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO.
Je wajua kuwa kilichopelekea SAMSONI mpaka kukamatwa na wafilisti na kumtoboa macho kilikuwa kipindi ambacho alikuwa akitafuta mchumba wa kuoa katika nchi ya wafilisti.SOMA  WAAMUZI 14;1,16:1-4,15,20.

C)WAKATI WA NDOA
Hiki ni kipindi cha kila mmoja kumuomba sana MUNGU kwaajili ya mwenzi wake,MME AU MKE wako anaweza akaua kusudi la MUNGU kwako kwa haraka sana.Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa mke ni mbeba maono au mkamilisha maono ya mwanaume,hivyo huyo msaidizi wako ni rahisi sana kuyafanikisha sana maono yako au ni rahisi sana kuyaua maono na makusudi ya MUNGU uliyoyabeba.AYUBU 2:9 Biblia inasema kuwa''NDIPO MKEWE AKAMWAMBIA JE WEWE HATA SASA WASHIKAMANA NA UTIMILIFUWAKO? UMKUFURU MUNGU,UKAFE.Mbeba maono na msaidizi wa Ayubu alimshaui ayubu kumtukana MUNGU ili afe kuliko kuteseka,NDUGU NAKUHAKIKISHIA KUWA AYUBU ANGEMSIKILIZA MKEWE NA KUMTUKANA MUNGU HISTORIA YAKE INGEISHIA HAPO NA MAKUSUDI YA MUNGU KWAKE YANGEISHA HAPO.
Wakati Mwanaharakati wa AFRIKA YA KUSINI   NELSON MANDELA  anapambana kuikomboa nchi yake alifungwa jela miaka 27 lakini mke wake alimvumilia na kumfariji mara kwa mara mpaka pale alipotoka gerezani na kuwa RAISI wa nchi hiyo.NAKUHAKIKISHIA KUWA MKE WAKE ASINGELIKUWA MBEBA MAONO NA MAKUSUDI YAKE MZURI ASINGELIKUWA RAISI WA AFRIKA KUSINI.
 KAFANYE UCHUNGUZE WATU AMBAO WAMEFANIKIWA SANA KATIKA MAENEO FULANI KAMA SIASA,BIASHARA,UCHUNGAJI,UONGOZI,UANDISHI WAKE ZAO WAMEKUWA MSAADA MKUBWA SANA KWAO KATIKA KUKAMILISHA MAKUSUDI YA MUNGU KWAO.

3.MANENO UNAYEJISIMEA MWENYEWE AU KUNENEWA NA WATU WENGINE
Ndugu yawezekana umekuwa ukijisemea maneno mabaya juu ya maisha yako kuwa mimi siwezi nikafanya hiki,fulani ndiye anayeweza kufanya ila sio mimi kuanzia leo acha tabia hiyo mara moja.KAMA MUNGU AMEKUPA KAZI YA KUFANYA NA WEWE UNASEMA MIMI SIWEZI UNATAKA NANI AFANYE HIYO KAZI WAKATI MUNGU AMEKUPA WEWE KUIFANYA? .YOELI 3:10b Biblia inasema''ALIYEDHAIFU NA ASEME MIMI NI HODARI.Hata kama unaona kazi ambayo MUNGU amekupa huwezi kuifanya usiseme kuwa huwezi bali fanya jitihada katika kuitimiza,

4.KUTENDA MAOVU
ISAYA 59:1-2 Biblia inasema'' TAZAMA MKONO WA BWANA HAUKUPUNGUKA,HATA USIWEZE KUOKOA WALA SIKIO LAKE SI ZITO HATA LISIWEZE KUSIKIA ,LAKINI MAOVU YENU YAMEWAFARAKANISHA NINYI NA MUNGU WENU NA DHAMBI ZENU ZIMEUFICHA USO WAKE MSIUONE HATA HATAKI KUSIKIA.
Maovu yetu huua kusudi la MUNGU ndani yetu maana MUNGU hupenda kuwapa kusudi lake wale wanaomtii na kuzishika sheria na Amri zake na kuzitenda.

5.KUKOSA MAARIFA/UFAHAMU
MUNGU akikupa kusudi lake inampendeza sana pale unapokuwa na maarifa na ufahamu katika kulifanikisha  kusudi lake,HOSEA 4:6  Inasema ''WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA;KWA KUWA WEWE UMEYAKATAA MAARIFA,MIMI NAMI NITAKUKATAA WEWE,USIWE KUHANI KWANGU MIMI.

6.KUKOSA MAONO( VISION)
Ndugu yangu kama hutakuwa na maono ya kubeba kusudi la MUNGU hakika kusudi la MUNGU kwako litakufa.MITHALI 29:18a  inasema''PASIPO MAONO WATU HUACHA KUJIZUIA''.HIVYO USIPOKUWA NA MAONO UTAKUWA SIO MTU WA KUJIZUIA MAANA UTAFANYA MAMBO KWA KWENDA PASIPO KUJUA UNAPOKWENDA NI WAPI.

7.MAJERAHA YA NAFSI NA KULIPIZA VISASI
Ndugu yangu huwezi ukatimiza kusudi la MUNGU kwako endapo wewe ni mtu uliyejaa na uchungu katika nafsiyako,hausamehi pale unapokosewa na kuwa mtu wa kulipiza visasi kwa watu pindi unapokosewa.WARUMI 12:17-19 inasema MSIMLIPE MTU OVU KWA OVU .ANGALIENI YALIYOMEMA MACHONI PA WATU WOTE,WAPENZI MSIJILIPIZE  KISASI BALI IPISHENI GHADHABU YA MUNGU MAANA IMEANDIKWA,KISASI NI JUU YANGU MIMI,MIMI NITALIPA,ANENA BWANA

8.RAFIKI YAKO
Rafiki yako wa karibu ni wa kuwa naye makini sana maana ni rahisi sana kuua kusudi la MUNGU aliloliweka katika maisha yako.MATHAYO 16:13-28
Hapa tunamuona PETRO aliyekuwa karibu sana na YESU akimkemea YESU kuwa aache kusema kuwa ATAKUFA wakati kusudi la MUNGU lilikuwa yesu afe kusudi MIMI na WEWE tuokolewe,hivyo YESU angemsikiliza PETRO hakika tusingelipata wokovu.

9.IMANI POTOFU(UGANGA NA UCHAWI)
Watu wengi wamepoteza makusudi ya MUNGU kwenye maisha yao kwa kuwategemea waganga kama suluhisho la Matatizo yao.YEREMIA 17:5 Inasema'' BWANA ASEMA HIVI  AMELAANIWA MTU  YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU ,AMFANYAYE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE NA MOYONI MWAKE AMEMWACHA BWANA''

10.ENEO/MAZINGIRA/MAHALI UNAPOISHI
usipokuwa makini Mazingira unayoishi ni rahisi sana kukufanya kuharibu kusudi la MUNGU kwako kutokana na watu unaoishi nao katika mazingira hayo,kuna wengine watakukatisha tamaa.wengine watakucheka kwa kila hatua unayojaribu kufanya na wewe utakubaliana nao na kukata tamaa na hatimaye kuua kusudi la MUNGU maishani mwako.

11.KIBURI KINACHOSABABISHWA NA VITU VIFUATAVYO;
A)uzuri wako wa sura au urembo wako,Akili yako au hekima yako,kipawa chako mfano sauti nzuri ya kuimba,cheo chako.
B)Fahari/utajiri wako/mafanikio yako ya kiuchumi,upako wako.
KUNA NA VITU HAPO JUU SI KOSA HATA KIDOGO NI FURAHA MBELE ZA MUNGU ENDAP UTAVITUMIA VIZURI ILA WATU WENGI WAKIWA NAVYO HUWADHARAU WENZAO SANA NA KUJIVUNA SANA KAMA VILE WAO NDIO KILA KITU NA KUMSAHAU ALIYEWAJALIA KUWA NAVYO.HIVYO HATIMAYE KUSUDI LA MUNGU KWA WATU KAMA HAO HUPOTEA KABISA KWAO


NDUGU USIKOSE MAKALA HIZI, TAMANI KUENDELEA KUZIPATA ILI UZIDI KUJIFUNZA ZAIDI.

KARIBU TENA SIKU NYINGINE ILI TUJIFUNZE HABARI MBALIMBALI

NA
SAMWEL MOHABE MARWA
samwelmarwa88@gmail.com
samwelmohabe.blogspot.com
P.O.BOX 65001
DAR ES SALAAM
0719200317/0745325174

AHSANTENI SANA
Monday, February 6, 2017

KINGDOM LEADERSHIP

*KINGDOM LEADERSHIP/UONGOZI WENYE DHANA YA UFALME WA MUNGU NDANI YAKE* *Watoto wa Jehova *ninawasalimia katika Jina la yesu kristo mwana wa Mungu aliyehai*🙌🙌✋� *Naomba tufuatane katika somo hili ili tujifunze kitu kupitia somo hili ,ninamuomba roho mtakatifu akupe Ufahamu ili uweze kuelewa somo hili* *kingdom leadership* *is the *kind of leadership* *that personifies the kingdom of God* *as demonstrated in the life and work of JesusChrist*. In *other words*, It's *leadership lifestyle* *that represents and manifests kingdom* *principles, policies and dictates* *contained in the* *Word of God*. *Uongozi wenye dhana ya Ufalme wa Mungu*Huu ni aina *ya uongozi ambao* *viongozi waliopo kusudi lao kubwa huwa ni kuudhirisha ufalme wa Mungu katika Maeneo wanayoongoza yaani kuuleta ufalme wa Mungu karibu na watu wanaowaongoza* *SIFA ZA KIONGOZI MWENYE DHANA YA UFALME WA MUNGU NDANI YAKE/KINGDOM LEADER* 1.Huwa *na *maono*/(vision) *ndani yake ,kiongozi mwenye dhana ya ufalme wa Mungu siku zote huwa na maono na kupitia maono hufanikanisha kusudi la Mungu alilomuitia na kumpa nafasi ya kuwa kiongozi,siku zote yeye huwa anaona kuna *Uwezekano*(Possibility) *haoni kutokuwezekana(Impossibility) hata kama wale anaowaongoza inafikia hatua wanakata tamaa Bali yeye huwa hakati tamaa hata kidogo Bali huwatia moyo wale anaowaongoza.* *Mithali 29:18* *Biblia inasema kuwa* *pasipo maono watu huacha kujizuia*viongozi wenye dhana ya ufalme wa Mungu ndani yao wanatakiwa kuwa na *maono* 2.Hana *dhana ya *umimi*(selfshiness ambition), *huwa anapeleka mbele mambo ya anaowaongoza mbele zaidi kuliko mambo yake yeye mwenyewe* kwenye kitabu cha kutoka 32:30-32 Biblia inasema *Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu,mmetenda dhambi kuu,na sasa nitakwenda juu kwa BWANA,labda niyafanya upatanisho kwaajili ya dhambi yenu.Musa akarejea kwa akasema ,Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.Walakini sasa,ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute nakusihi katika kitabu chako ulichoandika* *Musa angeliweza kumwambia Mungu awaangamize wanaisrael wote halafu Mungu amfanyie kizazi ambacho hakitamtenda dhambi ila alimwambia Mungu awasamehe watu wale wa Israel kwa sababu Musa alikuwa kiongozi aliye beba dhana ya ufalme ya Mungu ndani yake maana yake hakuwa na umimi* 3.Yuko *tayari kufa au kufungwa kwaajili ya watu anaowangoza/Ana sacrifice love kwa wale anaowaongoza* *YESU ni kiongozi aliyebeba dhana kubwa ya Ufalme wa Mungu maana alikubali *KUFA* *msalabani ili sisi wenye dhambi tuokolewe*. *Kutoka 32:32 Inasema, walakini sasa,ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute ,nakusihi katika kitabu chako ulichoandika* Musa *kwa sababu ni kiongozi aliye beba dhana ya ufalme wa Mungu ndani yake alimwambia Mungu kama hatawasamehe wana waisrael amfute katika kitabu cha uzima yaani alikubali kupoteza ufalme wa Mbinguni kwa sababu alikuwa kiongozi aliyebeba ufalme wa Mungu ndani yake* 4.Husikiliza na kuitii *sauti ya Mungu* *ukisoma kitabu cha 1 samwel 15,utakutana na habari za sauli alivyoambiwa na Mungu akaangamize ,akaue na akaharibu kila kitu nchi ya waameleki,Lakini sauli hakuitii sauti ya Mungu alipoenda Ameleki aliua ila hakumuua Mfalme wao AGAGI na hakuua wanyama wote Bali alichagua wanono ili akamfanyie Mungu sadaka ya kuteketezwa,kumtolea Mungu dhabihu na sadaka ya kuteketezwa ni wazo zuri lilikuwa ila siyo wazo la Mungu(IT'S GOOD IDEA BUT NOT GOD IDEA)* 5.Huenda na *ombi maalum mbele za Mungu(HE IS TOO SPECIFIC NOT TOO GENERAL)* *2 samwel 2:1 Inasema baada ya hayo,Daudi akauliza kwa BWANA ,akasema je ! Niupandie mji wowote wa Yuda ? BWANA akamwambia ,Haya panda.Daudi akasema ,Niupandie mji UPI ?Akasema Hebroni.Hapo tumeona kuna maswali mawili tofauti kumbuka Mungu anakujibu kama ulivyomuomba ,Mungu aliuliza swali la kwanza TOO GENERAL na Mungu naye alimjibu TOO GENERAL na swali la pili alivyokuwa SPECIFIC Mungu naye alimpa majibu SPECIFIC* 6.Hunyenyekea *Mbele za Mungu* *Kiongozi mwenye dhana ya ufalme wa Mungu ndani yake huwa Mnyenyekevu Sikuzote mbele za Mungu,huwa sio MTU wa kujisifu,dharau kwa wengine na m

KINGDOM LEADERSHIP

*KINGDOM LEADERSHIP/UONGOZI WENYE DHANA YA UFALME WA MUNGU NDANI YAKE* *Watoto wa Jehova *ninawasalimia katika Jina la yesu kristo mwana wa Mungu aliyehai*🙌🙌✋� *Naomba tufuatane katika somo hili ili tujifunze kitu kupitia somo hili ,ninamuomba roho mtakatifu akupe Ufahamu ili uweze kuelewa somo hili* *kingdom leadership* *is the *kind of leadership* *that personifies the kingdom of God* *as demonstrated in the life and work of JesusChrist*. In *other words*, It's *leadership lifestyle* *that represents and manifests kingdom* *principles, policies and dictates* *contained in the* *Word of God*. *Uongozi wenye dhana ya Ufalme wa Mungu*Huu ni aina *ya uongozi ambao* *viongozi waliopo kusudi lao kubwa huwa ni kuudhirisha ufalme wa Mungu katika Maeneo wanayoongoza yaani kuuleta ufalme wa Mungu karibu na watu wanaowaongoza* *SIFA ZA KIONGOZI MWENYE DHANA YA UFALME WA MUNGU NDANI YAKE/KINGDOM LEADER* 1.Huwa *na *maono*/(vision) *ndani yake ,kiongozi mwenye dhana ya ufalme wa Mungu siku zote huwa na maono na kupitia maono hufanikanisha kusudi la Mungu alilomuitia na kumpa nafasi ya kuwa kiongozi,siku zote yeye huwa anaona kuna *Uwezekano*(Possibility) *haoni kutokuwezekana(Impossibility) hata kama wale anaowaongoza inafikia hatua wanakata tamaa Bali yeye huwa hakati tamaa hata kidogo Bali huwatia moyo wale anaowaongoza.* *Mithali 29:18* *Biblia inasema kuwa* *pasipo maono watu huacha kujizuia*viongozi wenye dhana ya ufalme wa Mungu ndani yao wanatakiwa kuwa na *maono* 2.Hana *dhana ya *umimi*(selfshiness ambition), *huwa anapeleka mbele mambo ya anaowaongoza mbele zaidi kuliko mambo yake yeye mwenyewe* kwenye kitabu cha kutoka 32:30-32 Biblia inasema *Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu,mmetenda dhambi kuu,na sasa nitakwenda juu kwa BWANA,labda niyafanya upatanisho kwaajili ya dhambi yenu.Musa akarejea kwa akasema ,Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.Walakini sasa,ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute nakusihi katika kitabu chako ulichoandika* *Musa angeliweza kumwambia Mungu awaangamize wanaisrael wote halafu Mungu amfanyie kizazi ambacho hakitamtenda dhambi ila alimwambia Mungu awasamehe watu wale wa Israel kwa sababu Musa alikuwa kiongozi aliye beba dhana ya ufalme ya Mungu ndani yake maana yake hakuwa na umimi* 3.Yuko *tayari kufa au kufungwa kwaajili ya watu anaowangoza/Ana sacrifice love kwa wale anaowaongoza* *YESU ni kiongozi aliyebeba dhana kubwa ya Ufalme wa Mungu maana alikubali *KUFA* *msalabani ili sisi wenye dhambi tuokolewe*. *Kutoka 32:32 Inasema, walakini sasa,ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute ,nakusihi katika kitabu chako ulichoandika* Musa *kwa sababu ni kiongozi aliye beba dhana ya ufalme wa Mungu ndani yake alimwambia Mungu kama hatawasamehe wana waisrael amfute katika kitabu cha uzima yaani alikubali kupoteza ufalme wa Mbinguni kwa sababu alikuwa kiongozi aliyebeba ufalme wa Mungu ndani yake* 4.Husikiliza na kuitii *sauti ya Mungu* *ukisoma kitabu cha 1 samwel 15,utakutana na habari za sauli alivyoambiwa na Mungu akaangamize ,akaue na akaharibu kila kitu nchi ya waameleki,Lakini sauli hakuitii sauti ya Mungu alipoenda Ameleki aliua ila hakumuua Mfalme wao AGAGI na hakuua wanyama wote Bali alichagua wanono ili akamfanyie Mungu sadaka ya kuteketezwa,kumtolea Mungu dhabihu na sadaka ya kuteketezwa ni wazo zuri lilikuwa ila siyo wazo la Mungu(IT'S GOOD IDEA BUT NOT GOD IDEA)* 5.Huenda na *ombi maalum mbele za Mungu(HE IS TOO SPECIFIC NOT TOO GENERAL)* *2 samwel 2:1 Inasema baada ya hayo,Daudi akauliza kwa BWANA ,akasema je ! Niupandie mji wowote wa Yuda ? BWANA akamwambia ,Haya panda.Daudi akasema ,Niupandie mji UPI ?Akasema Hebroni.Hapo tumeona kuna maswali mawili tofauti kumbuka Mungu anakujibu kama ulivyomuomba ,Mungu aliuliza swali la kwanza TOO GENERAL na Mungu naye alimjibu TOO GENERAL na swali la pili alivyokuwa SPECIFIC Mungu naye alimpa majibu SPECIFIC* 6.Hunyenyekea *Mbele za Mungu* *Kiongozi mwenye dhana ya ufalme wa Mungu ndani yake huwa Mnyenyekevu Sikuzote mbele za Mungu,huwa sio MTU wa kujisifu,dharau kwa wengine na m