Saturday, April 29, 2017

MAJERAHA YA NAFSI PART TWO


KARIBUNI KATIKA SEHEMU YA PILI YA SOMO HILI

ZITAMBUE SIFA/TABIA  ZA NAFSI

Nafsi ni sehemu ya mwanadamu inayosababisha  mwanadamu kuwa hai,yaani kinachokufanya wewe ulivyo leo ni nafsi yako.
Mwanzo 2:7 Biblia inasema''Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu  akawa NAFSI HAI''

Zifuatazo ni sifa au tabia za   NAFSI

1.KWENYE NAFSI NDIPO KUNATOKA MAAMUZI YAKO WEWE(DECISION MAKING)

Zaburi 11:5 ''Bwana humjaribu mwenye haki bali nafsi yake humchukia asiye haki,na mwenye kupenda udhalimu''

kwenye nafsi ya mtu ndipo maamuzi hutokea,ndugu msomaji hakuna maamuzi yoyote uliwahi kuyafanya pasipo msukumo kutoka NAFSINI mwako,kama ulikuwa hujui tambua hilo leo.

Mwanadamu ameundwa na vitu vitatu ambavyo ni
A)MWILI
B)NAFSI
C)ROHO

Ndugu kuna muda unaweza kutamani jambo fulani baya katika maisha yako lakini nafsi yako ikakusuta na ukaacha kufanya hilo jambo,Wakati mwingine mwili ulikudanganya kuiba pesa kwa mtu fulani ,lakini nafsi yako ilisema hapana.Ukiona umemtamani mwanamke au mwanaume wa mtu ili uzini naye/ulale naye/ufanye naye mapenzi na ukafanikiwa kuzini naye jua kuwa hapo nafsi yako ilikuwa dhaifu kwenye maamuzi ,iko hivi mwili siku zote hutamani ukishindana na roho,hivyo kama MWILI ukiwa na nguvu kuliko ROHO hivyo nafsi hutekeleza matakwa ya mwili na kama  Roho itakuwa na nguvu kuliko vilevile nafsi itaamua matakwa ya Roho,NAFSI KAZI YAKE KUBWA NI KUFANYA MAAMUZI KATIKA YA ROHO NA MWILI NA KILE AMBACHO NAFSI HUTEKELEZA ADHIMA YAKE KAT YA ROHO NA MWILI JUA HICHO KINANGUVU KULIKO MWENZAKE.


2.KWENYE NAFSI NDIPO KUNATOKA FIKRA(MIND/UNDERSTANDING)

Mithali 23:7a ''Maana aonavyo NAFSINI mwake ndivyo alivyo''

Ukiona katika maisha yako unafikra mbaya juu yako mwenyewe au juu ya mwingine tambua kuwa nafsi yako haijakombolewa bado inahitaji kukombolewa.Yawezekana umewahi kuona kwa kuambiwa na nafsi yako kuwa huwezi kufanikisha jambo fulani hivyohivyo na wewe ukakata tamaa juu ya jambo hilo moja kwa moja.KINACHOTAKIWA KWENYE MAISHA YAKO NI KUIAMBIA NAFSI YAKO KUWA KILA KITU UNAWEZA HATA KAMA HUJUI JINSI YA KUKIWEZA.

Yoeli 10b 'ALIYEDHAIFU NA ASEME ,MIMI NI HODARI''.Hata kama ukiwa mnyonge na dhaifu iambie nafsi yako kuwa unaweza,nafsi huwa ya aina fulani kutokana na vyakula inavyolishwa mfano wewe kila siku ukilisha nafsi yako kuwa huwezi ndugu niamini HAUTAWEZA KWELI.Penda kulisha nafsi yako mawazo mema,mawazo ya ushindi na ya mafanikio,kuwa na tambia ya kuiambia nafsi yako kuwa kila jambo linawezekana na unaweza ukalifanya hata kama wengine hawakulifanikisha ,NAFSI MARA NYINGI HUDANGANYIKA BAADA YA KUONA MTU FULANI AMBAYE AMEFANYA JAMBO FULANI HALIJAFANIKIWA HUKULETEA PICHA KUWA WEWE HUWEZI HILI JAMBO MAANA FULANI LIMEMSHINDA WEWE UTAWEZAJE HIVYO HUKULETEA HOFU NZITO NA USIPOKUWA MAKINI NAFSI HUKUSHINDA

3.KWENYE NAFSI NDIPO  KUNATOKA HISIA (EMOTIONS/FEELINGS)

siku zote nafsi yako inapenda ipendwe,isifiwe,ipongezewe,ikubalike,ipewe fursa

Fuatilia mfano huu utaelewa kitu nasema ,UKIWA UNATEMBEA UKAPITA KATIKATI YA KUNDI LA WATU WAMEKAA WANAZUNGUMZA  KUKAWA KUNA MTU UNAMFAHAMU HALAFU UKAMSALIMIA KWA MARA YA KWANZA LAKINI YEYE AKAKAA KIMYA AIDHA KWA KUSIKIA AU KUTOKUSIKIA,UTAJARIBU KUPAZA SAUTI ILI AKUSIKIE,PALE AMBAPO HAKUKUJIBU NINI KILITOKEA NI JERAHA KATIKA NAFSI YAKO MAANA NAFSI YAKO HUJIONA KAMA UMEDHAURIKA,HAKUKUJALI,HAKUPENDI HAYO YOTE YANATOKEA MAANA NAFSI HUTAMANI KUFANYIWA MEMA ,KUJALIWA NA KUPENDWA.NDIO MAANA KATIKA KUNDI ULILOPITA KAMA KUNA WATU WANAFIKRA NZURI UTASIKIA WANAKUAMBIA USIJALI BWANA HAJASIKIA AU POLE HAJASIKIA.kwa nini watakwambia kwa sababu wanajua nafsi imetendewa vitu ambayo haipendi.



 VITU VINAVYOJERUHI NAFSI ZA WATU WALIOWENGI NA KUWAACHIA MAJERAHA


1.MAHUSIANO

Siku moja Dada mmoja aliniambia kuwa wanaume wote anawachukia na hataki hata kuwaona,Roho mtakatifu akaniambia kuwa amejeruhiwa nafsi yake na wanaume hao ndio maana hataki kuwaona.Ndipo nikapata ujasiri wa kumuuliza kwanini akaanza kunielezea namna ambayo kaka mmoja waliyekuwa wameahidfiana kuwa wachumba na wakawa wachumba kweli ila yule mkaka mwisho wa siku akamuacha yule mdada na akampata mdada mwingine hivyo nafsi ya dada yule ikajeruhiwa na ikamwambia fanya maamuzi ya kuchukia wanaume wote,kila mwanaume unayemuona dunia Muone kama kiumbe hatari kwako.


2.MARAFIKI
kuna watu wameumizwa nafsi zao kutokana na aina ya marafiki waliochagua kuwa nao katika maisha yao,kuna wengine marafiki zao walitembea na mume wake au mke wake,kuna wengine marafiki zao waliwashawishi kuwa na tabia za wizi,kuna wengine marafiki zao waliwasababisha wakafeli masomo yao,kuna wengine marafiki zao waliua ndoto zao walizokuwa nazo.Rafiki yako anaweza akawa Adui yako mkubwa au rafiki yako mkubwa maana huwa anajua siri zako kuliko mtu yeyote,huwa anajua maono na ndoto zako kuliko mtu yeyote hivyo kuwa makini katika uchaguzi wa marafiki la sivyo utapelekea nafsi yako kupata majeraha makubwa sana ambayo kuyaziba itahitaji muda mwingi na gharama nyingi sana

Zekaria 13:6''NA MTU ATAMWAMBIA ,JE JERAHA HIZI ULIZONAZO KAIKA YA MIKONO YAKO NININI,NAYE ATAJIBU,NI JERAHA NILIZOTIWA KATIKA NYUMBA YA RAFIKI ZANGU''



3.WAZAZI/WALEZI WAKO
kuna wengine nafsi zao zimejeruhiwa kutokana na malezi waliyoyapata kutoka kwa wazazi au walezi wao.Yawezekana ulikua katika mazingira ambayo wazazi wako wote walikuwa wamefariki,hivyo nafsi yako ikawa yamasononeko ,majonzi na huzuni muda wote  au kuna wengine ambayo wamelelewa na wazazi katika mazingira ya kuwabana sana(WATOTO WA GETI KALI)yaani haupati hata muda wakutoka ufurahi na wenzako,ucheke na wenzako ,uimbe na wenzako ,hivyo nafsi yako huwa ya kubanwa na uoga siku zote,Kumbuka nimekuambia nafsi hupenda kufurahi,kuchangamka na kuwa huru hivyo basi nafsi hujeruhiwa na wazazi.WEWE MZAZI UNAYESOMA UJUMBE HUU KUMBANA MTOTO WAKO NDANI YA GETI SIKU ZOTE SIO NJIA YA KUMFANYA MTAKATIFU AU YA KUMZUIA KUFANYA MAOVU BALI NI NJIA YA KUIANGAMIZA NAFSI YAKE NA KUATHIRI MFUMO WAKE WA FIKRA,NJIA RAHISI YA KUMFUNDISHA MWANAO KUACHA MAOVU NI KUMFUNDISHA NENO LA MUNGU KWA WINGI NA KUMUACHA KUWA HURU.




4.NDUGU ZAKO
Kuna watu wameumizwa na ndugu zao nafsi zao,na kupelekea muda mwingine kutokusalimiana,kuongea,kushiriki meza moja,kushiriki ibada moja,kushiriki chakula pamoja,kushikana mikono na kadhalika.ukiona watu kama hawa ikiwa ni wewe mwenyewe au katika jamii yako jua kuwa kuna watu nafsi zao zimejeruhiwa tayari



5.MUAJIRI WAKO
kuna watu ambao katika kazi zao kila siku wanamgogoro na muajiri wake,inaweza kuwa ni kwa sababu ya maslahi,wivu ,madaraka,mshahara au cheo.utakuta Bosi hawasalimiani na muajiriwa wake.ukiona watu kama hao kazi jua kuwa kuna mmoja wapo aidha BOSI AMA MUAJIRIWA AMEJERUHIWA NAFSI YAKE.



Vitu vinavyosababisha nafsi za waliowengi wengi kujeruhiwa ni vingi sana ila kwa leo naomba kuisha hapo.



ILI KUPONYA NAFSI INAHITAJI TUMUAMINI MUNGU KUPITIA MWANAYE YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU KWA SABABU NAFSI NI SEHEMU YA MWANADAMU AMBAYO MUNGU ALIIUMBA KWETU,HIVYO ILI IPONYE INAHITAJI MUUMBA WAKE AIPONYE.

Hosea 6:1 ''Njoni ,tumrudie BWANA;maana yeye amerarua,na yeye atatuponya ;yeye amepiga,na yeye atatufunga JERAHA ZETU''.


NINAWATAKIA USOMAJI MWEMA NA MUNGU WANGU AWABARIKI WOTE


MARWA SAMWEL M
0719200317/0745325174
samwelmarwa88@gmail.com
samwelmohabe.blogspot.com
P.O.BOX 65001
DAR ES SALAAM


GOD KINGDOM MINISTRY.

No comments:

Post a Comment