Friday, February 24, 2017

MAJERAHA YA NAFSI

KARIBU KWENYE SOMO HILI LA MAJERAHA YA NAFSI TUJIFUNZE WOTE.

NAFSI  ni ule uhai wa mtu (nafsi ndiyo wewe mwenyewe).Kinachokufanya kuishi wewe ni kwa sababu nafsi yako iko hai au ni kwa sababu nafsi yako inaishi.

Mwanzo 2:7 inasema Bwana akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai,mtu akawa nafsi hai

Yohana 10:11 inasema Mimi ndiye mchungaji  mwema.Mchungaji mwema huutoa UHAI wake kwaajili ya kondoo,YESU alisema kuwa yeye kwa sababu ni mchungaji mwema atatoa NAFSI yake au UHAI  wake afe kwaajili yetu wanadamu.

MAJERAHA ni ile hali mtu au kitu chochote kuumizwa na mtu mwingine au kitu kingine na kuachiwa maumivu makali sana ambayo ili kupona maumivu hayo mpaka yapewe tiba.

MAJERAHA YA NAFSI ni ile hali ya nafsi ya mwanadamu  au kitu chochote chenye nafsi  kuumizwa na mtu mwingine au kitu chochote ambapo ili majeraha haya yapone yanahitaji tiba.

KWANINI NIMEAMUA KUKULETEA SOMO HILI

Ndugu neno hili imekuwa msukumo mkubwa ambao MUNGU aliweka ndani yangu miaka 7  iliyopita tangu 2010 nikiwa   JIJINI MWANZA

ILIKUWA  mwaka 2010 mwezi wa 12 nikiwa MWANZA ambapo kuna dada mmoja aliyeitwa PILLY aliyekuwa ni mwanachuo wa chuo kikuu cha mtakatifu AUGUSTINO -MWANZA ,  Dada huyu alikuwa na kaka mmoja aliyeitwa kwa jina la JOSEPH watu hawa wawili waliahidiana kuoa yaani walikuwa wachumba wa Muda mrefu kama miaka 2 na alikuwa amebakiza mwaka wake wa mwisho wa kuhitimu elimu yake ya chuo kikuu.

SIKU moja huyo   mkaka alimwambia huyo mdada  kuwa yeye hayuko tayari kumuoa huyo binti .YULE BINTI baada ya kuambiwa hivyo alichukua uamzi wa kunywa sumu ili afe aondoke duniani maana aliona hana thamani tena hapa duniani akimkosa yule mkaka ,YULE MDADA ALIKUNYWA SUMU KWA SABABU NAFSI YAKE ILIKUWA IMEPATA MAJERAHA MAKUBWA( MAJERAHA YA NAFSI)
Ninamshukuru sana MUNGU kwa sababu  MUNGU alinitumia mimi kuokoa maisha ya yule dada,nilikuwa nipo nje ya Nyumba ambayo tulikuwa tunakaa ambapo mtoto mdogo wa miaka 9 alikimbia nje kwa haraka sana na kuniambia njoo uone dada ambavyo amekuwa.NDUGU nilivyoenda ndani yule mdada alikuwa akitoka MAPOVU  MDOMONI NA PUANI NA HUKU AKITAPIKA nikakimbia mpaka dukani kwa bwana mmoja aliyekuwa na duka jirani yetu kwa haraka sana pasipo hata hodi nikaingia ndani nikachukua MAZIWA pasipo hata kulipa pesa nikarudi kwa haraka sana huku ninakimbia ,Bwana aliyekuwa na duka alishangaa sana hali ile kwa siku ile na watu walinishangaa sana maana haikuwa kawaida yangu kufanya hivyo,Wengine walisema nimechanganyikiwa na kuwa kichaa KUMBE HAWAKUJUA NILIKUWA NAKIMBIA KUOKOA UHAI WA BINTI YULE.Nilipofika nilimnywesha MAZIWA yale kwa lazima ambapo alitapika ILE SUMU YOTE ALIYOKUWA AMEKUNYWA.Na baada ya tukio hilo nikampigia simu yule mkaka ALIYEMJERUHI i NAFSI YAKE NA KUMUELEZA YALIYOTOKEA AMBAPO ALIKUJA KWA HARAKA NA KUMPELEKA HOSPITALI.

MUNGU NI MWEMA yule dada alipona majeraha yake maana  yule mkaka aliyemjeruhi nafsi yake walisameheana  na kuoana  mwaka 28/4/2012 ambapo mpaka dakika hii ninayozungumza wana watoto wawili na wanaishi kwa furaha sana katika ndoa yao na wamekuwa mfano wa kuigwa katika jamii yao.
MTU MMOJA ASEME AMEN.


TABIA ZA MTU  ALIYEPATA MAJERAHA YA NAFSI

1.HUWA NA HASIRA AMBAZO HAZIISHI MUDA WOTE,mtu aliyejeruhusiwa nafsi yake huwa na hasira muda wote kwa watu wengine maana nafsi yake imeumizwa hata kumpelekea hasira
.
2. HUWA NA CHUKI.mtu aliyejeruhiwa nafsi huwa haishiwi na chuki muda wote huwa na chuki kwa  wenzake maana yawezekana wao ndio waliosababisha nafsi yake kuumizwa na hivyo huchukua uamzi wa kuwachukia ,muda mwingine hataki kuwaona.

3.HANA AMANI WAKATI WOWOTE,nafsi ya mtu iliyojeruhiwa na watu au kitu kingine tofauti na watu huwa haina AMANI hata kidogo.

4.HUWA NA UADUI,muda wote huwaona watu wengine maadui zake.

5.HASAMEHI WENGINE,Nafsi yenye majeraha huwa ni ngumu sana kutoa msamaha pale ambapo ukimkosea hata kidogo au hata kwa bahati mbaya.mfano unaweza ukamkanyaga mguu wake kwa bahati mbaya akakuchukia maisha yake yote.

6.HULIPIZA KISASI,mtu mwenye nafsi iliyojeruhiwa huwa ni mtu wa kulipiza visasi visasi siku zote.akikosewa kidogo hutafuta mbinu ya kulipiza kisasi.

7.HUWA NA WIVU USIOKUWA WA MAENDELEO.mtu aliyejeruhiwa nafsi yake huwa na wivu usiokoma nafsi mwake.ukitaka kufanikiwa kidogo hutafuta hata mbinu ya kuua mafanikio yako yako.

8.HANA FURAHA,nafsi iliyojeruhiwa siku zote huwa haina furaha maana huwa imejaa chuki,masimango,huzuni,hasira,masononeka,uadui na ugomvi muda wote.

9.HUWA HANA UVUMILIVU.mtu aliyejeruhiwa nafsi yake siku zote huwa si mtu wa kuvumilia mambo.

10.HANA HURUMA,nafsi yenye majeraha haiwi na huruma kwa wengine mfano kuna wengine waliopata ukimwi kwa bahati mbaya hivyo wanapogundua kuwa wanaishi na virusi vya ukimwi hufanya mbinu zozote hata kwa kubaka ili tu asife mwenyewe yaani aambukize na wengine.

11.HANA UPENDO.mtu ambaye amejeruhiwa nafsi yake tayari huwa si mtu wa upendo hata kidogo kwa wenzake maana huwaona wao kama visababishi vya majeraha yake hata kama si wao.

NDUGU UKIJIONA UNATABIA KAMA HIZO JUA NAFSI YAKO IMEJERUHIWA ,HIVYO ANZA KUPIGA HATUA YA KUIPONYA NAFSI YAKO ILI USIENDELEE KUISHI KWA MAJERAHA BALI UISHI KWA AMANI.
AYUBU 22:21 inasema kuwa mjue sana MUNGU ILI UWE NA AMANI NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUJIA

NDUGU UKIMUONA MWENZAKO ANATABIA KAMA HIZO JUA NAFSI YAKE IMEJERUHIWA HIVYO USIMCHEKE WA KUMUONGEA KWA WENZAKO BALI MSHAURI NA MUOMBEE MAANA WEWE NI SEHEMU KUBWA SANA KWAKE KATIKA KUPONYA NAFSI  YAKE ILIYOPATA MAJERAHA.

KUMBUKA UNAWEZA UKAJERUHIWA NAFSI YAKO NA BABA YAKO,MAMA YAKO,KAKA YAKO,DADA YAKO,MKE WAKO,RAFIKI YAKO,MPENZI WAKO,NDUGU YAKO WA KARIBU,JIRAHI YAKO ,MCHUNGAJI WAKO,WAFANYAKAZI WENZAKO NA HATA BOSI WAKO.

NJIA KUBWA YA KUSHINDA MAJERAHA YA NAFSI NI KUKUBALI KUSAMEHE WENGINE HATA KAMA WAMEKUKOSEA AU WAMEKUKWAZA,KUMBUKA USIPOKUWA MTU WA KUSAMEHE HUIBEBESHA NAFSI YAKO MZIGO MKUBWA WA CHUKI UNAOTEMBEA NAO HUKU UKIKUSUMBUA SIKU ZOTE.KUANZIA LEO ACHILIA WALE WOTE WALIOKUUDHI NAFSINI MWAKO ILI UISHI KWA FURAHA ,UPENDO NA AMANI.

TEMBELEA BLOG YANGU MARA KWA MARA ILI KUJIFUNZA MENGI .

EV.SAMWEL MOHABE MARWA
samwelmarwa88@gmail.com
samwelmohabe.blogspot.com
FB: SAMWEL MOHABE MARWA
0719200317
P.O.BOX 65001 DAR ES SALAAM,
TANZANIA



No comments:

Post a Comment