Friday, February 17, 2017

SABABU ZA KUSUDI LA MUNGU KUTOKUFANIKIWA KWA WATU

SABABU ZA KUSUDI   LA  MUNGU KUTOKUFANIKIWA KWA WATU 

Ninakusalimia katika JINA LIPITALO MAJINA YOTE AMBALO NI JINA LA YESU KRISTO.

KARIBU TUJIFUNZE TENA KATKA SEHEMU YA PILI YA KUSUDI LA MUNGU KWETU SISI WANADAMU.

Leo tutaangalia kuhusu sababu zinazopelekea kusudi la MUNGU ndani ya maisha yetu sisi wanadamu lisifanikiwe.Zifuatazo ni mojawapo ya sababu zinazopelekea kusudi la MUNGU lisifanikiwe kwetu wanadamu.

1.KUSUDI LA MUNGU KUFANYIKA KABLA AU NJE YA MUDA.
kuna watu ambao MUNGU ameweka vitu vikubwa ndani yao,ila vitu vinashindwa kufanikiwa pale ambapo mubeba kusudi anapotaka kufanya jambo hilo kabla ya wakati wake au baada ya wakati ule kuisha na yeye anajaribu kulifanya,yawezekana kusudi la MUNGU ni  kuwa kiongozi ,lakini umeshindwa kutambua nyakati na majira ambayo MUNGU amekuweka kuwa kiongozi ,hivyo ukilazimisha uwe kiongozi kabla ya wakati wako wa kuwa kiongozi haujafika utaharibu kusudi la MUNGU la kukuweka wewe kuwa kiongozi na pia ukifanya nje ya muda ambao MUNGU alikuweka uwe kiongozi unaharibu pia kusudi la MUNGU kwako maana MUNGU amepanga muda fulani uwe kiongozi na muda fulani usiwe kiongozi.
MHUBIRI 3:1-8 ,Biblia inaniambia kuwa ''kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.HIVYO WEWE MSOMAJI NINAKUSHAURI KUTAMBUA WAKATI UPI NI SAHIHI KWAKO KATIKA KULITIMIZA NA KULIFANIKISHA KUSUDI LA MUNGU KWAKO.

2.VIPINDI MUHIMU VYA MAISHA kama vile wakati wa ujana, wakati wa kutafuta mchumba na   wakati wa Ndoa
Hivi ni vipindi vya kuwa navyo makini sana ndugu msomaji maana vinaweza kuua kusudi la MUNGU haraka sana kwako
A)WAKATI WA UJANA
Kipindi cha ujana ni kipindi ambacho watu waslio wengi huharibu maono ya MUNGU na  makusudi ya MUNGU katika maisha yao ,maana hiki ni kipindi ambacho vijana huwakwa na tamaa za miili yao.Vijana huwa na tamaa na mihemko ya miili yao sana na wengi hujikuta wameingiza katika mtego wa ibilisi na kufanya uzinifu,NISIKILIZE KWA UMAKINI SANA NDUGU MSOMAJI YUSUFU ANGELIFANYA UZINZI NA YULE MKE WA POTIFA ASINGELIWEZA KUWA WAZIRI MKUU KATIKA MISRI,KILICHOSABABISHA YUSUFU AKATIMIZA KUSUDI LAKE LA KUWA WAZIRI MKUU KATIKA MISRI NI KWA SABABU ALIIKIMBIA DHAMBI YA UZINZI.soma Mwanzo  39:7-15
ushauri wangu kwenu ni kuwa hauwezi ukawa mzinifu halafu MUNGU akakuandaa kubeba kusudi lake kubwa kwaajili yako na kwaajili ya watu wake wengine.

B)WAKATI WA KUTAFUTA MCHUMBA
Nisikilize kwa umakini sana ndugu yangu,watu wengi wameshindwa kufanikisha kusudi la MUNGU katika Maisha yao kwa kujichanganya sana katika kipindi cha kutafuta mtu sahihi wa kuishi  naye kwa maisha ya baadaye yaani mke au mme ,watu wengi wanatafuta wachumba kwa akili zao wenyewe pasipo kumshirikishi MUNGU kumbuka MUNGU alimpa ADAMU  mkewe HAWA kama msaidizi wake hivyo nasi wanaume tunapotafuta MKE yapaswa tumuulize sana MUNGU kuhusu mke sahihi.NI HERI KUACHA KUOA KULIKO KUKOSEA KUCHAGUA MTU SAHIHI KATIKA MAISHA YAKO maana utakuwa na majuto katika maisha yako yote.MKE KAMA MSAIDIZI KWA MWANAUME NI WA KUJA KUBEBA MAONO YAKO  WEWE MWANAUME.HIVYO UKIKOSEA MUBEBA MAONO YAKO KBALIANA NA MIMI TU KKUWA KUSUDI LA MUNGU KWAKO HAKIKA HALITAFANIKIWA MAANA ANAYEBEBA MAONO YAKO NAYE HAJAKAA SAWA MAANA UTAPANGA KUFANYA HIVI ATAKUAMBIA HIYO HAIFAI NA UTAMSIKILIZA NA KUFANYA KINYUME NA KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO.
Je wajua kuwa kilichopelekea SAMSONI mpaka kukamatwa na wafilisti na kumtoboa macho kilikuwa kipindi ambacho alikuwa akitafuta mchumba wa kuoa katika nchi ya wafilisti.SOMA  WAAMUZI 14;1,16:1-4,15,20.

C)WAKATI WA NDOA
Hiki ni kipindi cha kila mmoja kumuomba sana MUNGU kwaajili ya mwenzi wake,MME AU MKE wako anaweza akaua kusudi la MUNGU kwako kwa haraka sana.Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa mke ni mbeba maono au mkamilisha maono ya mwanaume,hivyo huyo msaidizi wako ni rahisi sana kuyafanikisha sana maono yako au ni rahisi sana kuyaua maono na makusudi ya MUNGU uliyoyabeba.AYUBU 2:9 Biblia inasema kuwa''NDIPO MKEWE AKAMWAMBIA JE WEWE HATA SASA WASHIKAMANA NA UTIMILIFUWAKO? UMKUFURU MUNGU,UKAFE.Mbeba maono na msaidizi wa Ayubu alimshaui ayubu kumtukana MUNGU ili afe kuliko kuteseka,NDUGU NAKUHAKIKISHIA KUWA AYUBU ANGEMSIKILIZA MKEWE NA KUMTUKANA MUNGU HISTORIA YAKE INGEISHIA HAPO NA MAKUSUDI YA MUNGU KWAKE YANGEISHA HAPO.
Wakati Mwanaharakati wa AFRIKA YA KUSINI   NELSON MANDELA  anapambana kuikomboa nchi yake alifungwa jela miaka 27 lakini mke wake alimvumilia na kumfariji mara kwa mara mpaka pale alipotoka gerezani na kuwa RAISI wa nchi hiyo.NAKUHAKIKISHIA KUWA MKE WAKE ASINGELIKUWA MBEBA MAONO NA MAKUSUDI YAKE MZURI ASINGELIKUWA RAISI WA AFRIKA KUSINI.
 KAFANYE UCHUNGUZE WATU AMBAO WAMEFANIKIWA SANA KATIKA MAENEO FULANI KAMA SIASA,BIASHARA,UCHUNGAJI,UONGOZI,UANDISHI WAKE ZAO WAMEKUWA MSAADA MKUBWA SANA KWAO KATIKA KUKAMILISHA MAKUSUDI YA MUNGU KWAO.

3.MANENO UNAYEJISIMEA MWENYEWE AU KUNENEWA NA WATU WENGINE
Ndugu yawezekana umekuwa ukijisemea maneno mabaya juu ya maisha yako kuwa mimi siwezi nikafanya hiki,fulani ndiye anayeweza kufanya ila sio mimi kuanzia leo acha tabia hiyo mara moja.KAMA MUNGU AMEKUPA KAZI YA KUFANYA NA WEWE UNASEMA MIMI SIWEZI UNATAKA NANI AFANYE HIYO KAZI WAKATI MUNGU AMEKUPA WEWE KUIFANYA? .YOELI 3:10b Biblia inasema''ALIYEDHAIFU NA ASEME MIMI NI HODARI.Hata kama unaona kazi ambayo MUNGU amekupa huwezi kuifanya usiseme kuwa huwezi bali fanya jitihada katika kuitimiza,

4.KUTENDA MAOVU
ISAYA 59:1-2 Biblia inasema'' TAZAMA MKONO WA BWANA HAUKUPUNGUKA,HATA USIWEZE KUOKOA WALA SIKIO LAKE SI ZITO HATA LISIWEZE KUSIKIA ,LAKINI MAOVU YENU YAMEWAFARAKANISHA NINYI NA MUNGU WENU NA DHAMBI ZENU ZIMEUFICHA USO WAKE MSIUONE HATA HATAKI KUSIKIA.
Maovu yetu huua kusudi la MUNGU ndani yetu maana MUNGU hupenda kuwapa kusudi lake wale wanaomtii na kuzishika sheria na Amri zake na kuzitenda.

5.KUKOSA MAARIFA/UFAHAMU
MUNGU akikupa kusudi lake inampendeza sana pale unapokuwa na maarifa na ufahamu katika kulifanikisha  kusudi lake,HOSEA 4:6  Inasema ''WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA;KWA KUWA WEWE UMEYAKATAA MAARIFA,MIMI NAMI NITAKUKATAA WEWE,USIWE KUHANI KWANGU MIMI.

6.KUKOSA MAONO( VISION)
Ndugu yangu kama hutakuwa na maono ya kubeba kusudi la MUNGU hakika kusudi la MUNGU kwako litakufa.MITHALI 29:18a  inasema''PASIPO MAONO WATU HUACHA KUJIZUIA''.HIVYO USIPOKUWA NA MAONO UTAKUWA SIO MTU WA KUJIZUIA MAANA UTAFANYA MAMBO KWA KWENDA PASIPO KUJUA UNAPOKWENDA NI WAPI.

7.MAJERAHA YA NAFSI NA KULIPIZA VISASI
Ndugu yangu huwezi ukatimiza kusudi la MUNGU kwako endapo wewe ni mtu uliyejaa na uchungu katika nafsiyako,hausamehi pale unapokosewa na kuwa mtu wa kulipiza visasi kwa watu pindi unapokosewa.WARUMI 12:17-19 inasema MSIMLIPE MTU OVU KWA OVU .ANGALIENI YALIYOMEMA MACHONI PA WATU WOTE,WAPENZI MSIJILIPIZE  KISASI BALI IPISHENI GHADHABU YA MUNGU MAANA IMEANDIKWA,KISASI NI JUU YANGU MIMI,MIMI NITALIPA,ANENA BWANA

8.RAFIKI YAKO
Rafiki yako wa karibu ni wa kuwa naye makini sana maana ni rahisi sana kuua kusudi la MUNGU aliloliweka katika maisha yako.MATHAYO 16:13-28
Hapa tunamuona PETRO aliyekuwa karibu sana na YESU akimkemea YESU kuwa aache kusema kuwa ATAKUFA wakati kusudi la MUNGU lilikuwa yesu afe kusudi MIMI na WEWE tuokolewe,hivyo YESU angemsikiliza PETRO hakika tusingelipata wokovu.

9.IMANI POTOFU(UGANGA NA UCHAWI)
Watu wengi wamepoteza makusudi ya MUNGU kwenye maisha yao kwa kuwategemea waganga kama suluhisho la Matatizo yao.YEREMIA 17:5 Inasema'' BWANA ASEMA HIVI  AMELAANIWA MTU  YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU ,AMFANYAYE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE NA MOYONI MWAKE AMEMWACHA BWANA''

10.ENEO/MAZINGIRA/MAHALI UNAPOISHI
usipokuwa makini Mazingira unayoishi ni rahisi sana kukufanya kuharibu kusudi la MUNGU kwako kutokana na watu unaoishi nao katika mazingira hayo,kuna wengine watakukatisha tamaa.wengine watakucheka kwa kila hatua unayojaribu kufanya na wewe utakubaliana nao na kukata tamaa na hatimaye kuua kusudi la MUNGU maishani mwako.

11.KIBURI KINACHOSABABISHWA NA VITU VIFUATAVYO;
A)uzuri wako wa sura au urembo wako,Akili yako au hekima yako,kipawa chako mfano sauti nzuri ya kuimba,cheo chako.
B)Fahari/utajiri wako/mafanikio yako ya kiuchumi,upako wako.
KUNA NA VITU HAPO JUU SI KOSA HATA KIDOGO NI FURAHA MBELE ZA MUNGU ENDAP UTAVITUMIA VIZURI ILA WATU WENGI WAKIWA NAVYO HUWADHARAU WENZAO SANA NA KUJIVUNA SANA KAMA VILE WAO NDIO KILA KITU NA KUMSAHAU ALIYEWAJALIA KUWA NAVYO.HIVYO HATIMAYE KUSUDI LA MUNGU KWA WATU KAMA HAO HUPOTEA KABISA KWAO


NDUGU USIKOSE MAKALA HIZI, TAMANI KUENDELEA KUZIPATA ILI UZIDI KUJIFUNZA ZAIDI.

KARIBU TENA SIKU NYINGINE ILI TUJIFUNZE HABARI MBALIMBALI

NA
SAMWEL MOHABE MARWA
samwelmarwa88@gmail.com
samwelmohabe.blogspot.com
P.O.BOX 65001
DAR ES SALAAM
0719200317/0745325174

AHSANTENI SANA




1 comment:

  1. Amina
    Mungu azidi kukujaza maarifa yake
    na atupe Neema ya kulifuata neno lake!

    ReplyDelete